SIKU ZA DAYOSISI

Opublikowano: 2016-02-03 23:29:46

Utaishi kwa siku tatu na familia za wanaparokia ya Poznan katika eneo kubwa la Poland. Matukio yatakuwa mpangilio wa baraka za aina tatu kama ifuatavyo. 1. Wabarikiwa ni wale walio maskini kiroho. 2. Wabarikiwa ni walio safi mioyoni. 3. Wabarikiwa ni wale walio na huruma. Kwa hizo siku tatu mtasoma mila na tamaduni za wenyeji pamoja na kusali na vijana kutoka sehemu nyingi duniani na wale wa Dayosisi ya Poznan.

Utakuwa wakati mzuri wa kufurahia ukarimu wa watu wa Poland ambao umefurahiwa tangu karne za zamani. Kutakuwa na wakati wa kufurahia na majukumu ya kufurahia. Wikendi ya tarehe 23 na 24 Julai mtakusanyika pamoja na vijana wa Poznan, Poland, na wageni kutoka ughaibuni(nchi za ng'ambo.) Tarehe 23 mtaweza kuujua mji mkuu wa Greater Polandi kwa undani. Kuna maeneo mtakayozuru katika Parokia na kufurahia vyakula vya kienyeji. Jumapili kutakuwa na mashindano ya vijana. Misa Takatifu itakuwa mahali paitwapo Pilgrim Zone 'Jordan'. Baadaye kusali, kuabudu na tamasha.

Jumatatu 25 Julai kila mtu atasafiri hadi Krakow kwenye tamati ya sherehe na kukutana na Baba Mtakatifu.

Na hapa ni faida chache ya mkoa wetu na baadhi ya mapendekezo:

• Poznan imeshikana vema na Ulaya: uwanja wa kimataifa wa ndege katikati,kituo cha reli na masaa 3 kwenye basi kutoka Berlin. Ni kama kilomita 360 tu kutoka Krakov.

• Tutapeana usafiri au uchukuzi kwa mahujaji karibu na Dayosisi, na pia kusafirisha wanaoenda Krakov.

• Katika siku kabla ya "siku katika Dayosisi" tuna tayari mapendekezo kwa ajili ya safari kuzunguka Poland.

• Taizé Mkutano wa Ulaya ulifanyika katika Poznan katika mwaka 2009/2010.

• Mtakatifu papa Yohana II alizuru Poznan na maeneo mbalimbali mara kadha.

• Mtakatifu Faustina Kowalska aliishi,alifanya kazi na kuombea hapa.Ubatizo wa Poland ulifanyika miaka 1050 iliyopita karibu na Poznan. Hii ndio sababu ya Dayosisi yetu alichukua jina JORDAN.

• Tulikuwa moja ya miji ilioandaa kope la UEFA EURO waka wa 2012

Swali lolote elezwa: wyd@jordan-poznan.pl